Vikosi vya usalama nchini Somalia, vimesema dadi ya vifo vilivyotokana milipuko miwili katika mji wa Mahas uliopo eneo la kati jimbo la Hiram imeongezeka na kufikia watu 19.

Katika shambulizi hilo, watu kadhaa walijeruhiwa ambapo Afisa usalama wa mji huo, Abdullahi Adan amesema, shambulio hilo limetokea baada ya kutegwa kwa mabomu mawili ndani ya magari.

Watoa huduma za dharula wakiendelea kutoa msaada katika moja ya mashambulizi y amabomu nchini Somalia. Picha ya ABC.

“Magaidi hawa walishambulia mji wa Mahas asubuhi ya leo kwa kutumia mabomu yaliyotegwa kwenye magari, na ndicho kimesababisha watu 19 kufariki kwa nyakati tofauti,” amefafanua Adan.

Shambulizi hilo, ambalo limedaiwa kufanywa na wanamgambo wa Al Shabaab katika jimbo hilo la Hiram, ambalo awali operesheni kali ilifanywa dhidi ya kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.

Afande Sele apinga ujio wa Kocha Robertinho
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 5, 2023