Leo Ijumaa ndio siku ya kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ kusikiliza shauri la mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ na klabu ya Young Africans lakini kubwa zaidi ni namna wanasheria wa pande zote mbili wanavyopishana katika ofisi za TFF, Dar es Salaam.

Feisal na Young Africans wana mgogoro wa kimkataba ambapo kiungo huyo inaelezwa alivunja mkataba wake na Wanajangwani hao ili kuwa huru kujiunga na timu nyingine, huku Yanga ikidai bado ina mkataba naye.

Hadi kufika saa 10:40 Asubuhi, wanasheria wa Feisal na wale wa Young Africans wakiongozwa na Simon Patrick walikuwa katika viunga vya TFF wakisubiri kuanza kusikilizwa shauri hilo.

Kubwa zaidi ni namna walivyokuwa wakifanya mambo yao, tangu kuingia ambapo Simon wa Yanga aliingia na gari nyeupe akiwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Andrew Mtine mida ya saa 3:40 asubuhi.

Baada ya kufika TFF waliwakuta wale wa Feisal wakiwa wameingia nusu saa kabla lakini hata hivyo hawakusalimiana na kila pande kuendelea na mikakati yao.

Wakiwa katika viunga vya TFF muda mwingi walionekana kubaki kwenye magari yao bila kuyazima huku wakiendelea kusubiri kuanza kwa shauri hilo.

Wakati wakiendelea kusubiri, saa 4:22 aliingia Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Alex Mgongolwa na gari yake lakini hakutoa maelekezo yoyote kwa Wanasheria hao na kuendelea na mambo mengine ya kiofisi.

Hadi kufika saa 10:50 Asubuhi, shauri hilo lilikuwa halijasikilizwa na Feisal amefika Kwa kuchelewa maeno hayo ambapo amefika saa Tano na dakika kadhaa.

Ajali nyingine ya Basi: 16 wafariki, 21 majeruhi
Simon Msuva afunguka usajili wa Ronaldo