Kikosi cha Simba SC kimerejea jijini Dar es salaam kikitokea kisiwani Unguja (Zanzibar), baada ya kutolewa kwenye Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Simba SC imerejea Dar es salaam, tayari kwa maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City FC, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 17.

Maandalizi ya Kikosi cha Klabu hiyo ya Msimbazi kuelekea mchezo dhidi ya Mbeya City, yanatarajiwa kuanza mara moja baada ya kuwasili jijini humo, chini ya Kocha Mkuu Robertinho akisaidiana na Makocha Juma Mgunda na Seleman Matola.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil, aliwashuhudia baadhi ya wachezaji wa Simba SC kwenye Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023, na huenda akawa anajua pa kuanzia katika maandalizi ambayo yatakuwa na lengo la kuzinasa alama tatu muhimu dhidi ya Mbeya City.

Ikiwa Kisiwani Unguja (Zanzibar), Simba SC ilicheza Michezo miwili ya Kombe la Mapunduzi 2023, ikipoteza 0-1 dhidi ya Mlandege FC kisha ikaifunga KVZ 1-0.

Simon Msuva afunguka usajili wa Ronaldo
Feisal Salum aitikia wito TFF