Kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ ameitikia wito wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’, baada ya kutakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo leo Ijumaa (Januari 06).

Feisal amelazimika kufika mbele ya Kamati hiyo, baada ya kushtakiwa na Uongozi wa Young Africans kwa tuhuma za kutoroka Kambini sambamba na kuvunja Mkataba kinyume na Taratibu.

Kiungo huyo aliyesajiliwa Young Africans mwaka 2018 akitokea JKU ya nyumbani kwao Zanzibar, aliwasili katika Ofisi za Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ akiwa na mtu ambaye hakufahamika mara moja ni nani.

Baada ya kufika katika viunga vya ofisi za TFF, Feisal alikwenda moja kwa moja katika chumba maalum mbacho kinatukika kusikiliza kesi inayomkabili dhidi ya Uongozi wa Klabu ya Young Africans.

Desemba 23-2022 zilitoka taarifa za Fei toto kuandika Barua ya kuvunja Mkataba wake ndani ya Klabu ya Young Africans, ambapo tangu hapo hajaonekana kambini akitimkia kwao Zanzibar kabla ya hivi karibuni kusafiri kwenda Dubai kwa mapumziko.

Simba SC yarejea Dar, Robertinho kuanza kazi
Richard jela miaka 30 kwa ubakaji