Mtu mmoja, Richard Martin (42), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka binti wa miaka (11).

Martin ambaye ni mkazi wa kijiji cha Minjingu kilichopo Babati, Mkoani Manyara anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, 2022 katika kijiji cha Minjingu kilichopo jirani na Ziwa Manyara.

Richard Martin, akiwa chini ya ulinzi.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, Victor Kimario ilidaiwa kuwa mshtakiwa alimkuta mtoto huyo akiwa na kaka yake (14), wakichunga ng’ombe ndipo akaomba kusaidiwa kupakia gunia la mkaa, na wakiwa njiani Richard alimwambia kaka wa binti arudi kuangalia mifugo isipotee ndipo akapata mwanya wa kutenda tuko hilo.

Kabla ya hukumu, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Grace Mgaya aliiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho na Mshtakiwa akaomba kupunguziwa adhabu kwani ana watoto watatu ambao ni wadogo na mama yao alishafariki na wanamtegemea.

Feisal Salum aitikia wito TFF
Rais Samia ateuwa wengine sita