Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya, ambaye Januari 3, 2023 alimteua kuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Rais Samia amefanya utenguzi huo hii leo Januari 5, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Taaifa hiyo imezidi kufafanua kuwa, nafasi ya Diwani Athumani imechukuliwa na Mululi Mahendeka ambaye alikuwa ni Ofisa mwandimizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Januari 3, 2023, Rais Samia alimteua Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 6, 2023
Kamati za Kudumu kukutana kabla ya Bunge