Rais wa Kenya, William Ruto ametetea hatua yake ya kuagiza vyakula vilivyobadilishwa vinasaba (GMO), na kusema vyakula vyote ambavyo vimekuwa vikiagiza na nchi vina viambajengo hivyo ndani ya asilimia moja inayohitajika na ofisi ya ubora wa bidhaa Kenya (KEBS).

Ruto, ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na wanahabari katika Ikulu jijini Nairobi na kusema “Siwezi kuhatarisha maisha ya watu walionichagua mimi ni mwanasayansi, wanasayansi wote nchini wanakubaliana kwamba GMO haina madhara.”

Rais wa Kenya, William Ruto. Picha ya The Standard.

Kuhusu madai ya kuwepo kwa Ofisi ya Binti wa Kwanza kama mtoto wa Rais, Ruto amesema binti yake Charlene Ruto amefanya hafla na mikutano kadhaa ya hadhi ya juu chini ya jina hilo na kwamba katika sheria za Kenya, hakuna ofisi kama hiyo.

Amesema, “Mwache binti yangu Charlene, unajua hawa ni watoto, ni watoto tu, unajua kabisa kwamba hakuna ofisi kama hiyo. yeye ni bintiye William Ruto tu na wakati mwingine hajui mgawanyiko kati ya rais na baba.”

Kamati za Kudumu kukutana kabla ya Bunge
Binti kizimbani kwa mauaji Mhadhiri SAUT