Mfalme wa Ubelgiji Philippe Léopold na mkewe malkia Mathilde ni miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliofika katika uwanja wa mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya kushiriki misa ya mazishi ya Papa Benedict wa XVI.

Misa ya mazishi hayo, inayongozwa na Papa Francis ikiwa ni mara ya kwanza mazishi ya Papa wa zamani yanaongozwa na papa aliye madarakani huku waombolezaji wakifika uwanjani saa tano kabla ya kuanza kwa ibada.

Ibaada ya mazishi ya Papa Benedict wa XVI ikiendelea. Picha ya Guglielmo Mangiapane/ REUTERS.

Aidha, eneo linapofanyikia misa hiyo, linalindwa na zaidi ya maofisa wa usalama elfu moja wa Italia, walioitwa kutoa ulinzi kwa eneo hilo la mazishi huku Serikali ya Italia ikiagiza bendera zote nchini humo kuperushwa nusu mlingoti.

Papa Benedict wa XVI, amefariki akiwa na umri wa miaka 95 na akiwa kiongozi wa kwanza katika historia ya kanisa Katoliki Duniani kujiuzulu kwa sababu za kiafya katika kipindi cha miaka 600.

Binti kizimbani kwa mauaji Mhadhiri SAUT
Ruto akanusha kumtafutia kazi Odinga