Binti mmoja, Sarah Mwendesha (15), amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilemela kusomewa shitaka la mauaji ya aliyekuwa Mhadhiri wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mkoani Mwanza, Hamida Mussa.

Mshtakiwa huyo ambaye alikuwa ni msaidizi wa kazi za ndani, anadaiwa kumuua bosi wake Mhadhiri Hamida (Mama Mwakitosi), Novemba 29, 2022 kwa kumnyonga akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki akitumia mtandio.

Aidha, siku ya tukio baada ya kutekeleza mauaji hayo Sarah alitoroka kwenda Wilaya ya Misungwi na alikamatwa na Polisi siku tatu baadaye kisha kufunguliwa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja.

Hata hivyo, kesi yake imetajwa na kuahirishwa hadi Januari 19, 2023 itakapoitwa kwa ajili kutajwa tena na mshtakiwa hukuruhusiwa kuzungumza chochote kwani Mahakama hakuwa na mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.

Siwezi hatarisha maisha ya walionichagua: Ruto
Maelfu wahudhuria ibada mazishi ya Papa Benedict wa XVI