Wakati mashabiki wa Chelsea wakiendelea kuuguza kidonda cha kupokea kipigo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Crystal Palace klabu ya Chelsea imepokea habari mbaya nyingine baada ya idadi ya majeruhi kuongezeka.
Mchezaji Victor Moses ameungana na Alvaro Morata na Ng’olo Kante katika orodha ya majeruhi wa Chelsea baada ya Mnigeria huyo kuumia katika mchezo dhidi ya Crystal Palace.
Moses atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne ambazo ni sawa na mwezi mmoja hali itakayompelekea kukosa mchezo kati ya Chelsea na Manchester United ambao utapigwa tarehe 5 mwezi ujao
-
Harry Kane, Ronaldo nani kuibeba timu yake leo?
-
Tanzania na Kenya zashuka viwango vya FIFA, Ujerumani, Brazil za paa juu
-
Jose Mourinho asema hatastaafu akiwa Man Utd
Moses atakosa jumla ya michezo saba ikiwemo michezo miwili ya Champions League dhidi ya As Roma na pia Bournemouth, Watford, Everton,Manchester United na West Bromich Albion.
Habari hizi zinaweza kuwa njema kwa mchezaji mpya wa Chelsea David Zapaccosta kwani anaonekana anaweza kuwa mtu sahihi kuziba pengo la Victor Moses ambaye msimu huu ulianza vizuri kwake.
Wakati huo huo Chelsea watakuwa uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge siku ya Jumatano ambapo wataikaribisha As Roma katika muendelezo wa michuano ya Champions League