Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaendelea usiku wa leo huku mchezo unaovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ukiwa ule utakaopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu wakati Real Madrid watakapochuana na Tottenham.

Kikubwa kinachozungumzwa kwa wadau wa mchezo wa soka ni kukutana kwa Cristiano Ronaldo na mchezaji wa Spurs, Harry Kane ambao wanakaribiana kwa uwiano wa kufunga magoli katika kundi lao.

Kane amefunga jumla ya mabao matano katika michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya wakati Ronaldo ametupia magoli manne katika michezo miwili ya kundi H.

Kitu kingine kinachofanya mchezo huo kuwa gumzo na kuvutia zaidi ni pale Luka Modric na Gareth Bale watakapocheza dhidi ya Tottenhamambayo ni klabu yao ya zamani.

Ronaldo na Kane wotw wamefunga mabao 43 katika klabu zao na timu za taifa mwaka huu. Kane amefunga mabao 15 ktika michezo14 huku Ronaldo akifunga mabao 10 katika michezo 12 msimu huu.

Kingine kitakacho vuta hisia kwa mashabiki ni kufuatia mabingwa hao wa tetezi wa klabu bingwa barani Ulaya Madrid kuhitaji kumsaini mchezaji wa Spurs, Harry Kane

Whatsapp yamponza Mbunge
NEC yaruhusu leseni ya udereva kupigia kura