Klabu ya Majimaji imeshushwa daraja na kufungiwa kucheza ligi kwa misimu miwili baada ya kushindwa kufika katika mchezo wake wa hatua ya mtoano ‘Play Off’ dhidi ya Kasulu United ya Kigoma.

Timu hiyo ya mkoani Ruvuma ilikuwa inashiriki First League ambapo ilikuwa imalize mchezo wa marudiano kwenye hatua ya mtoano ‘Play Off’ dhidi ya Kasulu United lakini haikuweza kusafiri kwa madai ya ukata wa fedha pamoja na kuahirishwa mara kwa mara.

Awali, mechi hiyo ilikuwa ipigwe kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Aprili 18, kisha kusogezwa siku tatu mbele, lakini viongozi kupitia chama cha soka Wilaya ya Songea (SOREFA) waliomba kupelekwa tena hadi Aprili 29, lakini hata hivyo haikuweza kufika uwanjani.

Katibu wa chama hich SOREFA Godi Mvula amesema kutokana na ukata walionao hadi kushindwa kusafiri, wanasubiri uamuzi wowote kutoka kwenye mamlaka za soka.

Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi na bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB) imefafanua kuwa kwa sababu mchezo huo ulikuwa wa ‘Play Off, jambo hilo linatafsiriwa kikanuni kuwa ni kujitoa kwenye ligi.

“Baada ya Majimaji kujitoa na kwa mujibu wa kanuni ya 31;4 (4.1) klabu hiyo inakabiliwa na adhabu ya kushushwa daraja na kufungiwa kucheza ligi kwa misimu miwili,” imeeleza taarifa hiyo.

Polisi yanasa mzigo wa Sigara za Bangi ukisafirishwa
Kocha Simba SC aipa heshima Azam FC