Katika Ulimwengu huu, watu wana uwezo wa kuishi miaka mingi endapo watazingatia njia kadhaa za kimaisha ambazo utazifahamu kupitia andiko hili, ingawa kwa mwaka 1950, iliarifikwa kwamba wastani wa maisha ya binadamu duniani ilikuwa ni kuishi miaka 46.
Hata hivyo, kwa baadhi ya mataifa mchakato huo wa maisha huwa sio rahisi kwani maradhi na matukio yasiyotarajiwa huwa yanawakumbusha watu kwamba maisha yana ukomo, kutokana na uwepo wa sababu nyingi za vifo ikiwemo ugaidi, vita na majanga ya asili na havipungui asilimia 0.5 ya vifo vyote duniani.
Taarifa za watu kufa, huwa zinategemea simulizi za namna vifo hivyo vinavyotokea na muda na takwimu zinaonesha kuwa takribani watu milioni 56 duniani kote walikufa kwa mwaka 2017 pekee, idadi ambayo ni milioni 10 zaidi ya watu waliokufa mwaka 1990.
Lakini jambo hili linaenda sambamba na idadi ya watu duniani kote, ambayo inaongezeka na watu huishi miaka mingi zaidi kwa wastani kwani zaidi ya watu asilimia sabini hufa kutokana na magonjwa yasioambukiza na ya muda mrefu.
Ugonjwa ambao unaua watu wengi ni shambulio la moyo, ukiathiri moyo na mishipa na idadi ya vifo vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo ni mara mbili na vinavyosababishwa na saratani, ugonjwa ambao ni wa pili kwa kusababisha vifo kwani kila vifo sita, kimoja kinakuwa kimesababishwa na saratani.
Magonjwa mengine ni kisukari, magonjwa yanayoadhiri mfumo wa kupumua na ugonjwa wa akili pia ambao upo kwenye orodha ya juu ya magojwa yanayosababisha vifo, huku jambo ambalo linastaajabisha likiwa ni idadi ya watu ambao wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika.
Taarifa zinaeleza kuwa, takribani watu milioni 1.6 walikufa kutokana na ugonjwa wa kuhara mwaka 2017, na hii inaweka ugonjwa huo kuwa ni miongoni mwa sababu 10 zinazosababisha vifo na katika baadhi ya nchi, ugonjwa huo unauwa watu wengi zaidi.
Magonjwa ya ulemavu wa watoto unaosababisha vifo vya watoto chini ya siku 28, pia ilikuwa ni sababu ya vifo milioni 1.8 vilivyotokea mwaka 2017 ingawa vifo vya mara kwa mara huwa vinatofautiana baina ya nchi moja na nyingine.
Nchi ya Japan, watoto wapatao 1,000 wanakufa chini ya siku 28 baada ya kuzaliwa ukilinganisha na nchi 20 zilizo masikini na magonjwa mengine yanaweza kuzuilika ikiwemo ajali za barabarani zinazosababisha vifo vingi katika nchi maskini na tajiri, kwani vifo milioni 1.2 vilisababishwa na ajali kwa mwaka 2017.
Hata hivyo, nchi ambazo zina watu wenye kipato kikubwa, vifo vinavyotokea kwenye nchi hizo zinatokana na ajali za barabarani katika miongo ya hivi karibuni, lakini ajali hizo pia huwa ni za barabarani na karibu mara mbili ya vifo vinatokana na wale wanaojiua au kuuwana.
Nchini Uingereza, vifo vya watu kujiuwa iko juu mara 16 vikiwa ni vya watu wenye umri unaokadiriwa kuwa ni kati ya miaka 20-40 na kupungua kwa vifo vya watoto ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika huduma ya afya duniani.
Aidha, kuna mafanikio makubwa katika janga la magonjwa ya maambukizi kwa mfano janga la maambukizi ya virusi vya ukimwi ambayo yaliwekewa juhudi kubwa katika kufanikisha zinapatikana dawa za kufubaza makali ya Virusi hivyo na kusaidia anguko la namba za vifo Duniani.
- Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya Habari.