June 31, 2007 Rais wa Zamani wa Libya, hayati Moummar Gaddafi akiwa amesindikizwa na Walinzi wake wa kike waaminifu, alihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Afrika – AU, jijini Accra nchini Ghana.

Siku hiyo, alikuwa amevalia Shati lake la Khaki lenye Picha za Wapiganaji na Waasisi wa Mataifa ya Afrika wenye Misimamo Mikali (Pan Africanists), kama Patrice Lumumba, Abdul Nasser, Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkurumah, Nelson Mandela, Sekou Toure, Thomas Sankara n.k.

Gaddafi akasema, “ndugu zangu Waafrika, tunapaswa kuchagua moja aidha kuiunganisha Afrika yetu au kuruhusu ife, tunapaswa kuwa na Muunganiko wa Mataifa ya kiafrika na kuunda (United States of Africa), tuna kila kitu ndani ya Bala hili sasa ni vema tukaitimiza Ndoto hii, kwa kuwa wamoja tunaweza kupambana na Ulimwengu wa kileo.”

Kanali Muammar Gaddafi, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mapinduzi ya Libya, Tripoli Sept 2, 2009. Picha ya Steve Bent.

Lakini miaka kadhaa Baadaye, Gaddafi ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Afrika Mstaafu (AU), alivamiwa pale Libya, akauawa pale pale Libya kwa kile kilichopambwa na Mabeberu huku Ulaya na Amerika kwa neno “DIKTETA”, neno ambalo mara zote Mabeberu na Vibaraka wamekuwa wakulitumia dhidi ya Viongozi wote wa Mataifa Machanga wanaojaribu kujinasua ktk Mtego wa Ukoloni wa Kiuchumi.

Kabla ya kuuawa kwa Ghaddafi, Libya ilikuwa na Fedha Nyingi kuliko idadi ya Wananchi wake, walikula na Kusaza na hata Fedha nyingine zikaelekezwa kuufadhili Umoja wa Afrika -AU, posho zote za vikao na mishahara ilitoka Libya, fedha ya Libya ikafadhili Miradi mbali Mbali ya Maendeleo Afrika Nzima.

Hikutosha, bado Mabilioni ya Dollar yakatumika kumaliza ghasia za vita nchini Niger na Mali, huku baadhi ya misaada tuliyopata Tanzania kama nchi ni pamoja na kujengewa Msikiti pale Dodoma (Msikiti wa Gadafi), uliopo jirani na Uwanja wa Mtekelezo au Uwanja wa Jamhuri.

Walinzi waaminifu Wanawake shupavu walikuwa wakimlinda Kanali Muammar Gaddafi

Leo Raia wa Libya wanasaga meno kwa kujutia uamuzi wao, waliyakataa maisha ya kifahari waliyoishi, maisha ya kupewa mishahara bila kufanya Kazi, kupewa mke na kulipiwa mahari na hata kupewa nyumba ili waanze Maisha.

Leo waweza kusema Libya ina laana, Damu ya Gaddafi na Chozi la Gaddafi juu ya ardhi yao, ni wapi kwenye raha? Sirte? Tripoli au Benghazi? jibu ni hakuna maana ni vurugu tupu na laana hiyo ya Gaddafi haijaliacha Bara la Afrika salama.

Kwanza ilianzia kwa Walibya na Sasa inagusa na Nchi zingine, yaani Binadamu anauzwa dollar 400 haijalishi ni Profesa ama Memkwa, ana uwaraza, kiduku ama Zazuu, Walibya Wamechanganyikiwa!

Kanali Muammar Gaddafi wakati alipokuwa akihutubia moja ya Mikutano nchini Nigeria.

Bila shaka unajiuiliza kivipi? Soma kwa umakini…… Biashara hii ya Utumwa wa mtu mweusi ni ya kulaaniwa na hata ingekuwa ya mtu mweupe ni laana pia, sasa tunauzana wenyewe kwa wenyewe, hii ni kupitia baadhi ya miradi yenye masharti yasiyo rafiki, mikopo kandamizi kwa baadhi ya nchi nk.

Bila shaka ni wakati Sahihi kuingilia kati baadhi ya mambo kwa Viongozi wetu kusimama kidete na kama Afrika na Viongozi wake wakikaa kimya wakajifungia majumbani mwao bila kutoka kauli wakati wa kusaini mikataba au miradi wanayoitilia mashaka basi tutakuwa tunatenda dhambi kubwa isiyofutika vizazi hata vizazi.

Kanali Muammar Gaddafi.

Kuna msemo unasema ‘Wema hawana maisha marefu’ japo kiuhalisia haina uthibitisho lakini wale wanaowatetea wanyonge mara nyingi ndio wanaowakandamiza, lakini ubaya wao hujulikana mapema kwani Nyeupe na Nyeusi huwa havikai nyumba moja.

Lakini hapa kuna swali la msingi ambalo huenda ndiyo ulozi wenyewe …. je? NI NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGELE?

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 23, 2023
Rasmi Tanzania yafungua Ubalozi wake Indonesia