Watu wengi hushika au kuwa na pesa mfukoni lakini hawafahamu mambo mengi juu ya pesa, wakati yapo mambo mengi ya kuyahafamu kuhusu hitaji hilo muhimu linaloendesha maisha ya mwanadamu.
Wahenga walipata kusema, ‘Ukiona vyaelea jua vimeundwa’ kwani kuna watu waliumiza vichwa kuhakikisha jambo linatokea ambalo litaifanya Dunia kuwa na usawa pale ambapo kupitia umiliki wa pesa basi utaheshimika popote ila ni mpaka uitafute upambane ama kwa elimu ama kwa kufanya kazi.
Waswahili nao wahajabaki nyuma, nao wanazidi kuboresha misemo eti wanasema ‘Ukiona Mbwa juu ya Mti kuna Mtu kampandisha’ wanadai kuwa Mbwa hana uwezo wa kupanda mti hivyo kuna raia tu atakuwa kahusika kama ilivyo kwa pesa kwamba mpaka ipo vile ilivyo kuwa watu lazima walisumbua vichwa.
Nimetangulia kusema hayo kwa kuwa hapa nataka kukuelimisha mambo machache ambayo pengine unayafahamu au huyafahamu au utaongeza ufahamu juu yake, nikianza na jambo la kwanza kuwa Pesa ya noti huwa siyo karatasi bali malighafi iliyotengenezea pesa hiyo, mojawapo ni pamba ambayo huifanya kuwa imara.
Jambo la pili ni kwamba, mgunduzi wa mashine ya kutolea pesa ‘ATM’, John Shepherd-Barron alipata wazo hilo akiwa bafuni na hiyo ilikuwakipindi cha miaka ya 1960 na kuanzia hapo alianza kuaanda mkakati kazi, ili kuhakikisha wazo lake linaleta matokeo na hadi sasa watu wanatumia ATM kwa madaha.
Pesa pia inadaiwa kuwa zina virusi vya mafua na dawa za kulevya, kwani watafiti wanasema wamebaini pesa hupita kwenye mikono na sehemu mbalimbali, na kwamba nyingi kati ya hizo huwa zina virusi vya mafua na chembechembe za madawa ya kulevya (cocaine), hivyo kwa akili ya kawaida vitakasa mikono ni muhimu sana.
Aidha, jambo la nne usilolifahamu ni kwamba, watu wote walio hai kwasasa nao walizikuta pesa zikitumika katika utaratibu huu tulionao, kwani inaaminika kuwa pesa zilianza kutumika miaka ya 5,000 K.B. (Kabla ya Kristo), hivyo ni wazi kuwa nao wataondoka na kuziacha, je? nani alitengeneza pesa.
Kitu cha tano ni kuwa, asili ya pesa za noti ni nchini China, ikiaminika kuwa noti zilibuniwa huko mwaka wa 910 na pesa hizi zilimshangaza mfanyabiashara wa Kiitaliano, mpelelezi na mwandishi kutoka Jamhuri ya Venice, Marco Polo wakati alipotembelea nchini humo.
Inaaminika kuwa utengenezaji pesa ni taaluma ngumu, yaani watu wengi wanafahamu kuwa ili usome udaktari au wanasheria unahitaji miaka mitano hadi sita kufuzu taaluma hizo, lakini utengenezaji wa pesa unahitaji si chini ya miaka 15 ili kufuzu, na ndio maana ni vigumu sana kutengeneza pesa bandia ambazo haziwezi kutambulika.
Pesa ni kitu muhimu ambacho wanadamu wamejiwekea kuwa kinakubaliwa kama njia ya malipo ya bidhaa na upataji wa huduma na ulipiaji wa mahitaji, kama vile chakula, mavazi na malazi katika nchi fulani au muktadha wa kijamii na kiuchumi Ulimwenguni.
Kiilikuwa jambo hili ni la kuibuka ambalo lilikuwa na thamani ya na karibu mifumo yote ya kisasa ya pesa inategemea pesa ambazo zinatambulika kuwa na thamani ya matumizi ambayo inatokana na utaratibu wa kijamii, baada ya kutangazwa na serikali au taasisi ya udhibiti kuwa ni halali.
Ugavi wa fedha wa nchi unajumuisha sarafu zote zinazotumika (noti na sarafu zinazotolewa kwa sasa), vilevile aina moja au zaidi ya pesa za benki (salio lililo katika akaunti za hundi, akaunti za akiba na aina nyinginezo za benki katika akaunti), thamani yake iko kwenye vitabu vya taasisi za fedha na zinaweza kubadilishwa kuwa noti halisi au kutumika kwa malipo yasiyo na pesa taslimu, huunda sehemu kubwa zaidi ya pesa pana katika nchi zilizoendelea.