Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani amewataka wananchi na wanasiasa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2020 ili kupata viongozi bora na waadilifu.
Amesema hayo wakati akizundua jengo la Taasisi ya kuzui na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Ambapo amewatahadharisha wanasiasa na wananchi dhidi ya vitendo vya Rushwa.
Naye Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jeneral John Mbungo amemueleza Makamu wa Rais kuhusu matokeo ya tume iliyoundwa ili kuchunguza tahamani ya fedha katika ujenzi wa ofisi hizo na hatua zilizochukuliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora keptaini mstaafu George Mkuchika amewataka TAKUKURU kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa licha ya kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.