Katika kuhakikisha Sekta ya Utalii Nchini Inapewa kipaumbele na kutangazwa kwa ajili ya manufaa ya taifa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amevitaka vyombo vya habari nchini kutangaza vivutio vilivyopo kwa manufaa ya taifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano kituo kimoja cha televisheni hapa nchini, amesea kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kutangaza utalii na kuweza kutoa habari ambazo zitasaidia kutoa muongozo kwa wageni na wenyeji.

Amesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaotembelea vivutio hivyo ni watu kutoka nje ya nchi hivyo amewaasa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ili waweze kuvielewa na kuwa mabalozi wazuri wa nchi yao.

“Ninaomba vyombo vya habari viwe na uzalendo wa kutangaza vivutio vyetu tulivyo navyo, kwani vikifanya hivyo vitakuwa vimelisaidia Taifa kujitangaza na kuongeza uchumi kupitia Sekta ya Utalii,”amesema Makani.

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania ni sehemu pekee duniani ambayo ni Chimbuko la Zamadam hasa katika eneo la Olduvai na Laetoli ambako kuna masalia ya Zamadam na Nyayo za kale.

Hata hivyo, kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete amesema kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa sana katika kutangaza utalii wa nchi kwani vikiamua kufanya hivyo vitavutia watalii wengi zaidi kutoka nchi za nje.

 

LIVE: Rais Magufuli akizindua Mabweni mapya ya Wanafunzi UDSM
Video: Jinsi mauaji ya kutisha ya Polisi 8 yalivyofanyika, Polisi yavaa sura mpya