Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa anatamani ifikapo mwaka 2020 majimbo yote ya mkoa wa Dar es salaam yawe yamerudi mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa amekuwa akipokea maombi mengi ya wabunge kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutaka kujiunga CCM.
Ameyasema hayo jijini Dar es salama wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Salenda, ambapo amesema kuwa kwasasa kuna wabunge na madiwani wengi kutoka Chadema wamekuwa wakiomba kujiunga CCM.
“kilichotokea Temeke ni toba, Ukonga ni toba, kilichotokea Kinondoni ni toba na huku kwenye kata kuna toba nyingi sana zinafanyika, kwa uungwana huu 2020 kitaeleweka.”amesema Makonda
Hata hivyo, ameongeza kuwa ameombwa na wengi kujiunga CCM, wakiwemo madiwani na wabunge wa Ubungo na Kibamba ambapo amedai kuwa wamehoji kuhusu tarehe ya mwisho wa kujiunga imeshapita lakini akawaambia ataongea na katibu mkuu kuuliza kama kuna usajili wa dirisha dogo.
-
Video: Makonda awalipua Chadema ‘Wameshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu yao’
-
Mnyika amshukuru JPM, ‘Watanzania wanakuombea usiwe na kiburi’
-
Video: Kubenea amfungukia JPM,’Nakuunga mkono kwa asilimia 200%’