Mahakama ya Kinondoni, imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mwanahabari Saed Kubenea dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ya matumizi mabaya ya madaraka.
Hakimu Mfawithi, Aroni Lyamuya amesema mbali na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yake, pia Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Amesema makosa yaliyotajwa hayaipi Mahakama hiyo uwezo wa kuyashughulikia, hali inayofanya Paul Makonda kuwa huru kutokana na kukosa kesi ya kujibu.
Saed Kubenea, kupitia jopo la mawakili wake alimstaki Paul Makonda katika kesi ya jinai no 7 ya mwaka 2021 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Watuhumiwa wengine walioshtakiwa na Mwanahabari huyo ni Mkurugenzi wa mastaka na DCI.