Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo mchana kwa saa Afrika mashariki limepanga makundi ya michuano ya Europa League msimu wa 2018/19, katika halfa maalum iliyofanyika mjini Monaco nchini Ufaransa.
Hatua ya upangaji wa makundi ya michuano hiyo imekamilika, baada ya kutanguliwa na ile iliyofanywa jana jioni ya kupanga makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Klabu ya Chelsea imeepuka kupangwa katika kundi gumu kama ilivyokua inatarajiwa na wadau wengi wa soka duniani, huku wawakilishi wengine wa England klabu ya Arsenal ikiwekwa kundi moja na Sporting CP ya Ureno.
Klabu nyingine zilizopangwa kundi moja na Arsenal ni FK Qarabag na FC Vorskla.
Chelsea (The Blues) wamepangwa katika kundi L, lenye timu za PAOK, BATE Borisov na Vidi FC.
Katika kundi hilo The Blues wanatarajia kukutana na wachezaji waliowahi kuitumikia Arsenal kama Chuba Akpom na Alex Hleb ambao wanazitumikia klabu za PAOK na BATE.
Klabu Celtic ya Scotland, imeangukia katika kundi B lenye timu za FC Salzburg, RB Leipzig pamoja na Rosenborg ambayo inatumikiwa na mshambuliaji Nicklas Bendtner, ambaye aliwahi kucheza nchini England akiwa na klabu za Arsenal, Nottingham Forest na Birmingham City.
Gwiji wa soka nchini England Steven Gerrard ambaye kwa sasa ni meneja wa klabu ya Rangers ya Scotland, atapambana na Villarreal, Rapid Vienna na Spartak Moscow katika michezo ya kundi G.
Makundi ya michuano ya Europa League kwa ujumla, baada ya kupangwa leo mchana na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.
KUNDI A: Bayer Leverkusen, Ludogorets, FC Zurich na AEK Larnaca
KUNDI B: FC Salzburg, Celtic, RB Leipzig na Rosenborg
KUNDI C: Zenit St Petersburg, FC Kobenhavn, Bordeaux na Slavia Prague
KUNDI D: Anderlecht, Fenerbahce, Dinamo Zagreb na Spartak Trnava
KUNDI E: Arsenal, Sporting Club, FK Qarabag na FC Vorskla
KUNDI F: Olympiacos, AC Milan, Real Betis na F91 Dudelange
KUNDI G: Villarreal, SK Rapid Wien, Spartak Moscow na Rangers
KUNDI H: Lazio, Marseille, Eintracht Frankfurt na Apollon Limassol
KUNDI I: Besiktas, Genk, Malmo na Sarpsborg 08 FF
KUNDI J: Sevilla, FC Krasnodar, Standard Liege na Akhisarspor
KUNDI K: Dynamo Kyiv, FC Astana, Stade Rennais na FK Jablonec
KUNDI L: Chelsea, PAOK, BATE Borisov na Vidic FC