Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameagiza kuondolewa kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania – TPDC, kutokana na kushindwa kutoa taarifa mbalimbali na kutofanya mikutano na wananchi wanaozunguka miradi ya Gesi Asilia ikiwemo dharura zinazotokea katika Mkuza wa Bomba la Gesi.

Dkt. Biteko ametoa maagizo hayo hii leo Novemba 14, 2023 wakati aliposimama katika Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara, Mkoa wa Mtwara ili kuzungumza na wananchi akiwa anatokea kukagua visima vya kuzalisha na mitambo ya kuchakata Gesi ya Mnazi Bay iliyopo katika Kata ya Msimbati wilayani humo.

Wananchi wa Kata ya Msimbati walimweleza Dkt.Biteko kuhusu changamoto walizonazo ikiwemo barabara, kituo cha afya, kutopata fedha zozote kutokana na kazi za uzalishaji wa uchakataji Gesi Asilia unaofanyika kwenye kijiji hicho na kutopata taarifa mbalimbali za mradi ikiwemo zinapotokea changamoto kwenye bomba la Gesi Asilia.

“Changamoto kwenye miradi hii zinatokea lakini lazima awepo mtu ambaye ni daraja kati ya Serikali na Wananchi, na Mtu huyu analipwa mshahara kwa kazi hiyo, haiwezekani Waziri au Rais kuja kutoa taarifa kwa wananchi wakati kuna mtu kaajiriwa kwa kazi husika, wananchi hawa wanapaswa kupata taarifa.” Amesisitiza Dkt.Biteko.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 15, 2023
WhatsApp yaboresha mazungumzo ya sauti