Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa Malaria bado ni changamoto nchini na kwamba katika kipindi cha miaka mitatu kati ya wagonjwa 100 waliofika kupata huduma kwenye vituo vya afya kumi walikua wa Malaria.

Waziri Ummy, amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga Mradi wa Okoa Maisha uliokua unatekelezwa katika Mikoa yenye maambukizi makubwa na kuzindua miradi miwili ya Shinda Malaria na Dhibiti Malaria.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2020 katika kila wagonjwa 100 waliolazwa kwenye vituo vya afya 16 ni wa Malaria, ambapo kwa mwaka 2021 ni wagonjwa 13 na 2022 ni wagonjwa 12.

Miradi hiyo ilitozinduliwa, inafadhiliwa na Program ya Malaria ya Rais wa Marekani (PMI), ukigharimu shilingi bilioni 45 kwa kipindi cha miaka minne.

Dkt. Mpango mgeni rasmi utalii Kimataifa
Wanahabari wasisitizwa ushirikiano uhuru wa vyombo vya Habari