Zaidi ya shule 400 nchini Malaysia katika mji wa Johor zimefungwa baada ya wanafunzi 75 kuumwa, kutapika na kupata matatizo ya kupumua.
Shule hizo zilizofungwa zipo katika eneo la viwandani, na uongozi wa eneo hilo umesema watatoa muongozo siku ya alhamis baada ya uchunguzi juu ya uchafuzi wa mazingira katika eneo hilo.
kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na chombo cha habari cha Bernama zinaeleza kuwa miongoni mwa shule zilizofungwa 100 ni za elimu ya awali na elimu ya sekondari pamoja na shule za chekechea 300.
Waziri Mkuu Sahruddin Jamal amesema kuwa wanafunzi 75 kutoka katika shule 15 waliopatwa na matatizo ya kupumua na waliokuwa wakitapika wamepelekwa hospitali kwa matibabu.
Sahruddin amewaambia waandishi wa habari kuwa bado haijawekwa sawa nini chanzo cha watoto kuumwa, japo amesema kuwa mlipuko huo hauna uhusiano na ule wa mwezi wa tatu ambao ulipelekea zaidi ya shule 111 kufungwa na maelfu ya watu kuumwa kwa kuchafuliwa na kemikali kwa mto wa Kim kim.
-
Video: Mazingaombwe ya AJABU zaidi Duniani | Hawa Wamefariki dunia wakionyesha Mazingaombwe yao LIVE
Waziri huyo ameahidi kuwa upelelezi utakapo kamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakao kutwa na hatia.
Ikumbukwe kuwe mnamo mwezi Machi mwaka huu maelfu ya watu nchini Malaysia walipata maumivu ya kifua na kutapika baada ya tani 40 za kemikali kumwagwa kinyume cha sheria katika mto Kim kim.
Na tayari watu watatu walitiwa hatiani ambao wawili ni wa nchi hiyo Malaysia na mmoja ni wa nchini Singapore.