Mali imemtangaza waziri wake wa zamani wa ulinzi Bah Ndaw kuwa Rais wa serikali ya mpito pamoja na kiongozi wa kijeshi kanali Assimi Goita kuwa Makamu wa rais wa nchi hiyo.
Tangazo hilo limetolewa baada ya Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi (ECOWAS), yenye mataifa 15 wanachama kutoa siku kadhaa kwa watawala wa kijeshi wa Mali kuwateua viongozi wa kiraia, ikionya kwamba haitaviondoa vikwazo vyake endapo hatua hiyo haitotekelezwa.
Uteuzi huo wa Mali utaweza kuendeleza mahusiano madhubuti na jeshi pamoja na uwepo wa shinikizo la kimataifa la kuteuliwa kwa kiongozi raia baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo ni marufuku ya kibiashara na kufunga mipaka, katika kipindi ambacho kilizongwa na mapinduzi ya Agosti 18, ambayo yalimuondoa madarakani rais Ibrahim Boubakar Keita.