Inaarifiwa kuwa, mwaka wa 1998, zaidi ya walimu 8,000 wa shule za Siberia na Urusi walilipwa kwa chupa 15 za mvinyo badala ya fedha kwa sababu mamlaka hazikuwa na uwezo wa kulipa mishahara yao.
Chupa hizo za mvinyo zilikuwa ni malipo ya miezi miwili na Walimu waliamua kuuza mvinyo huo ili kupata pesa na wengine kubadilishana kwa chakula.
Hatua hiyo ilitokana na kuyumba kwa uchumi wa Mataifa hayo mwanzoni mwa mwaka 1990 hadi mwaka 1998 na kusababisha maeneo hayo kupitia kipindi kigumu kuwahi kutokea.
Unayaonaje malipo na vipi ikitokea kwa wakati huu tena kibongo bongo?