Amri ya kutotoka nje katika mji wa Kherson ulioko karibu na eneo la mapambano kusini mwa Ukraine, imetolewa kwa saa 58 kuanzia Ijumaa jioni ya Mei 5, 2023

Amri hiyo imetolewa Mei 3, 2023 na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kherson, Oleksandr Prokudin, wakati ambapo vikosi vya Ukraine vikijiandaa na mashambulizi ya kupambana na vikosi vya Urusi majira ya machipuko.

Produkin amesema katika muda huo, ni marufuku watu kutembea kwenye mji huo. Aidha, raia watatu wameuawa katika shambulizi la Urusi lililotokea leo kwenye soko kubwa katika mji wa Kherson.

Wakati huo huo, Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, FSB, imesema kuwa watu saba wanaohusishwa na shirika la kijasusi la Ukraine wamekamatwa katika jimbo la Crimea.

Matumizi nishati safi: Mitungi 100,000 kutolewa bure
Malipo ya Mvinyo badala ya pesa yalivyolibua simanzi