Mchungaji Docho Eshete ameshambuliwa na kuuawa na mamba wakati akibatiza waumini katika ziwa Ayaba lililopo kusini mwa Ethiopia.
Wakati akianza kumbatiza mfuasi wa kwanza tu kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo katika ziwa Ayaba gafla mamba aliruka nje kutoka majini na kumchukua mchungaji huyo ambaye licha ya kujitahidi kupambana na kujiokoa na mashambulizi aliuawa na mamba huyo.
Juhudi za watu waliokuwepo eneo hilo ikiwa ni pamoja na wavuvi waliojaribu kutumia nyavu ili kumuokoa na mamba huyo asimwingize kwenye kina kirefu hazikuweza kuokoa maisha ya mchungaji huyo na walichoweza ni kuupata mwili wake baada ya kuwa tayari amefariki.
Uvuvi wa kupindukia unaosababisha idadi ya samaki ambacho ni chakula cha mamba kupungua utajwa kuwa sababu ya mamba kutoka ziwani na kuonekana mara kwa mara wakiwinda kando kando ya ziwa wakivamia watu na kuwaua.