Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ungwemgongo na wanyama wasio na ungwemgongo, ubongo unapatikana katika kichwa ukilindwa na mfupa ya fuvu.
Kazi kubwa ya ubongo ni kuhakikisha viungo muhimu vya mwili kama vile moyo na mapafu vinafanya kazi ipasavyo.
Hapa chini ni baadhi ya mambo muhimu kufahamu kuhusiana na ubongo.
- Ubongo wa binadamu huwa hauna vipokezi vinavyohusika na maumivu hivyo hauhisi maumivu kabisa, hivyo mtu anaweza kufanyiwa upasuaji wa ubongo huku akiwa na ufahamu wake na asihisi maumivu yeyote.
2. Ubongo ndiyo kiungo pekee cha mwili ambacho hutumia nguvu nyingi sana, zaidi ya asilimia 20 ya nguvu zote za mwili hutumiwa na ubongo japokuwa ubongo una asilimia mbili tu za uzito.
3. Zaidi ya asilimia 60 ya ubongo wa binadamu huwa umeundwa kwa mafuta huku asilimia 75 ya uzito wa ubongo inabebwa na maji.
4. Sehemu ya ubongo iitwayo NEOCORTEX ambayo huhusika na lugha pamoja na ufahamu ndiyo sehemu kubwa zaidi kuliko sehemu zote zinazounda ubongo, huchukua zaidi ya asilimia 76 ya ubongo wa binadamu hivyo kumfanya binadamu awe tofauti na wanyama wengine katika kuwaza kunena na kutenda.
5. Kila sehemu ya ubongo hufanya kazi jambo hili humfanya binadamu asiweze kutumia ubongo wake kikamilifu, inasadikika kuwa binadamu hutumia chini ya asilimi 10 tu ya ubongo wake.
6. Homoni inayoitwa Oxytocin ambayo hujulikana kama homoni ya mapenzi huzalishwa kwa wingi kwenye ubongo, na hupatikana kwa wingi katika matukio makuu matatu, matukio ya mapenzi ambapo homoni hii ndiyo huamua umpende nani, umpende vipi wakati gani utayapeleka vipi mapenzi yenu, na hii homoni ndio huamua umpende nani kwa wingi lakini pia homoni hii huzalishwa wakati wa kukutana kimwili mwanaume na mwanamke, lakini pia wkatati wa uchungu wa kuzaa homoni hii ndiyo huanzisha uchungu wa kuzaa, na la mwisho homini huongoza na kulinda mfumo mzima wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
7. Tukiwa kwenye ufahamu wetu, ubongo huzalisha kati ya watts 10 hadi 23 za umeme ambao unatosha kabisa kuwasha taa moja ya umeme.
8. Kupiga miayo hutokea mara nyingi baada ya kumuona mtu mwingine kafanya hivyo hi ni kwa sababu ubongo huwa na seli zinazoitwa seli kioo mirror cells, sehemu hii ya ubongo huigiliza kitendo hiki kutoka kwa mwingine na kitokea imeharibikabasi humfanya mtu awe na matatizo makubwa kata kuhsuiana ama kuishi na banadam mwingne
9. Ubongo huwa na mishipa ya fajamu zaido ya bilioni 100 hii ni mara 15 zaidi ya idadi ya watu wote tuliopo duniani.
10. Mziki husisimua sehemu ileile ya ubongo ambayo hutoa kemikali za raha Dopamine wakati wa kujamiana na kula.