Ni wazi kwamba timu ya Manchester United msimu uliopita wamefanya vibaya na kukosa mafanikio kwani waliweza kumaliza msimu bila kuambulia chochote ambapo walikosa mataji yote yakiwemo ligi kuu Uingereza, taji la Carling Cup,FA,UEFA na hata pia wamekosa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya ndani ya msimu ujao.
Uongozi wa timu hiyo kwa kuliona hilo sasa wameonekana kuweka nguvu katika suala la kusuka upya kikosi hicho ili kuweza kurudi kwenye makali yake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo imaripotiwa mchezaji wa timu hiyo Andreas Pereira huenda akapewa mkataba mpya utakao mfanya adumu kwenye klabu hiyo hadi mwaka wa 2023.
Gazeti la The Sun limeripoti kwamba endapo mchezaji huyo atapewa mkataba mpya utaupiku mkataba wa sasa ambao unatarajiwa kuisha Machi mwakani, baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer hapo awali kufanikisha jitihada za kumfanya mchezaji huyo adumu ndani ya timu hiyo hadi sasa.
Imeripotiwa kuwa Solksajer anapambana ili kumbakiza mchezaji huyo kwa muda mrefu ikiwezekana hadi kufikia miaka minne ijayo aendelee kuitumikia timu hiyo.