Mabingwa wa Soka Afrika Kusini Klabu ya Mamelodi Sundowns wamepangwa kuialika Simba SC katika michuano maalum ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/23.
Mamelodi Sundowns imepanga kuzialika timu tatu kutoka nje ya Afrika Kusini, ambazo zitatoa ushindani wa kweli kwenye michuano hiyo itakayopigwa kwa juma moja.
Kwa mujibu wa Meneja mawasiliano wa klabu ya Mamelodi Sundowns Shupi Nkgadima amesema maandalizi ya michuano hiyo yanakwenda vizuri na wanaamini yatazisaidia timu shiriki kwa ajili ya msimu ujao.
Klabu nyingine zinazotajwa kuwa kwenye mpango wa kualikwa ni Mabingwa mara tano wa Afrika TP Mazembe kutoka DR Congo na Al Hilal ya Sudan. Michuano hiyo inatarajia kuanza rasmi Julai 29.
Simba SC imewahi kuandaa michuano kama hiyo (Simba Super Cup) iliyochezwa mapema Mwaka 2021 jijini Dar es salaam, huku timu za TP Mazembe na Al Hilal zikialikwa.