Uongozi wa Singida Big Stars umeitaka Klabu ya Simba SC kutoa kiasi cha shilingi milion 35 ili wamuachie Mshambuliaji Habib Kyombo, aliyekamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo leo Jumanne (Juni 21).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars Muhibu Kanu amesema, Mshambuliaji huyo ni mchezaji wao halali, na kilichokua kikiendelea kati yake na Simba SC hakikuwa kinatambulika kisheria.

Amesema wanaamini Kyombo alidanganywa na baadhi ya watu, hadi kufikia hatua ya kuzungumza na viongozi wa Simba SC, huku ikielezwa alikaribia kusaini na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Kama Simba itakuwa tayari kutupatia kiasi cha Sh35 milioni ambacho tulimpatia Kyombo tunaweza kukaa nao meza moja kwa ustaarabu na tukawaachia mchezaji aende kucheza kwao,”
.
“Jambo kama hili limewahi kutukuta Singida wakati wa nyuma kwa Feisal Salum tulimsajili ila mwisho wa siku tulikubaliana na Yanga walitupatia gharama zetu na akaenda kucheza kwao na yupo huko hadi sasa.”

“Ila tumefanya utambulisho wa Kyombo leo baada ya kufahamu Simba imemsaini tayari mkataba wa miaka miwili wakati hapo awali alianza kusaini kwetu Singida nahisi kuna watu walimshauri vibaya, ila kwetu tulimpatia pesa hiyo na alishatumia kwenda kufanya mambo yake.” amesema Muhubu Kanu

Kyombo anamalizia mkataba wake na Mbeya Kwanza FC aliyoitumikia msimu huu 2021/22 kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Mamelodi Sundowns yaiita Simba SC Afrika Kusini
Vijana waupa kisogo uchaguzi Kenya