Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, imesema idadi ya wapiga kura vijana waliojiandikisha katika uchaguzi wa Agosti nchini Kenya imepungua tangu ikilinganishwa na uchaguzi wa miaka mitano iliyopita, hali inatajwa kuchangiwa na kukata tamaa kutokana na matatizo ya kiuchumi na ufisadi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati amesema licha ya watu waliojiandikisha kupiga kura kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 12, imesema baada ya ukaguzi wa sajili ya wapigakura imegundua kuwepo kwa pungufu hiyo.

“Kutakuwa na wapiga kura milioni 22.1 kwenye daftari lakini dadi ya vijana waliojiandikisha kupiga kura 2022 imefikia asilimia 39.84 ambayo ni kupungua kwa asilimia 5.27 dhidi ya 2017,” mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema.

Ameongeza kuwa, kulingana na takwimu za Serikali inaonesha Vijana wenye umri wa chini ya miaka 35 ni robo tatu ya wakazi wa Kenya wapatao milioni 50, na kwamba Wanawake wamekuwa na uwakilishi mdogo katika sajili ya wapigakura huku idadi yao ikichukua asilimia 49 ya jumla yote.

Kenya iliyo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa na nguvu ya kiuchumi, itafanya uchaguzi wa Rais na wabunge Agosti 9, 2022 chini ya kivuli cha chaguzi zilizopita ambazo mara nyingi zimekumbwa na ghasia za kikabila.

Ikiwa na idadi tofauti ya watu na makundi makubwa ya wapiga kura, Kenya kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na ghasia za kijamii zilizochochewa kisiasa wakati wa uchaguzi, hasa baada ya kura ya maoni ya 2007 ambapo zaidi ya watu 1,100 walikufa.

Wapiga kura wengi vijana wanaonyesha kutokuwa na shauku ya uchaguzi wa mwaka huu, wakiwa wamekatishwa tamaa na wasomi wengi wa kisiasa wanaoonekana kuwa wazembe na wafisadi.

Wakati wa ukaguzi huo, zaidi ya wapiga kura 246,000 waliofariki waliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura, huku Mwenyekiti wa IEBC akibainisha kuwa wametoa takwimu hizo katika hali ya uwazi na kujitolea kwa imani ya umma katika sajili ya wapiga kura.

Kinyang’anyiro cha urais mwaka huu kinaelekea kuwa na mbio za watu wawili wenye wafuasi wengi ambao ni Naibu Rais William Ruto (55), na Raila Odinga (77), ambaye ni mwanasiasa mkongwe na Waziri Mkuu wa zamani.

Singida Big Stars yaitikisa Simba SC
Barbara: Simba SC haijafeli usajili, tulieni mtaona