Lydia Mollel – Morogoro.
Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira, imeziagiza Mamlaka za Maji Mkoani Morogoro kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinazohusika na utunzaji pamoja na uhifadhi wa vyanzo vya Maji, kuja na mipango madhubuti ya kulinusuru Bwawa la Bindu pamoja na vyanzo vyake vinavyoingiza maji, dhidi ya uharibifu wa Mazingira.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Bwawa la Mindu, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amesema watafanya kila jitahida kuhakikisha fedha za mradi utakaonza mwezi april mwakani wa kuongeza tuta haitosua bali fedha zitafika kwa wakati kwani wanataka kuhakikisha changamoto ya maji inaisha kabisa morogoro.
UWT yampa agizo Mkandarasi ujenzi mradi wa Maji
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Maji na Mazingira, Felix Kavejuru amesema ni vyema Mamlaka hizo zikaungana kwa pamoja kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji, pamoja na bwawa hilo katika kutoa huduma ya Maji Safi na salama kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam malima amesema changamoto katika eneo hilo la mindu ilikiwa ni mikanganyiko wa wananchi kuondoka ndani ya mita 500 za bwawa hilo kwani badhi yao awakurudhishwa na upimaji wa eneo lakini watawashirikisha wadadu mbalimbali na wananchi wenyewe ili kujirizisha na wapishe katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasi amesema licha ya eneo la bwawa la mindu kuwa na changamoto ya miamba, wanajitahidi kupanda miti mingi ili kutunza mazingira lakini pia wanajitahidi kuwaondoa wananchi wanaoshi katika eneo hilo kinyume cha sheria.
Kamati hiyo, pia imeiagiza Serikali kuharakisha fedha za mradi wa upanuzi wa bwawa la mindu ili kusaidia utekelezaji wake kukamilika kwa wakati kama inavyokusudiwa kwenye malengoya mradi na ifahamike kuwa Bwawa la mindu linategemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro katika upatikanaji wa huduma ya Maji Safi na salama kwa zaidi ya asilimia 75.