Klabu ya Manchester City itamkosa kwa wiki nne mshambuliaji wake Sergio Aguero ambaye amepata ajali ya gari na kuvunjika mbavu.

Aguero alipata mpasuko katika mbavu kufuatia ajali ya gari aliyoipata akiwa mjini Amsterdam nchini Uholanzi alipokwenda kuhudhuria tamasha la muziki na atakosa mchezo kati ya Man City na Chelsea utakaopigwa leo.

Manchester City ambayo inaongoza ligi kuu ya Ungereza ikiwa na ponti 16 baada ya kucheza michezo 6 itachuana na Chelsea leo katika uwanja wa Etihad.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mshambuliaji huyo ameandika ujumbe akisema anaendelea vizuri na amewashukuru mashabiki wote waliopma pole na kumtakia afya njema

I’m home in Manchester after an exam by club Drs. It’s a broken rib. Hurts, but I’m fine, fully focused on recovery. Thank you all! pic.twitter.com/uamK7xwo99

— Sergio Kun Aguero (@aguerosergiokun) September 29, 2017


Video: Matonya ndani ya tuhuma, atajwa Diamond na Ney wa Mitego, Team Mtaa kwa Mtaa wafunguka

Barcelona warudi tena mahakamani kuhusu Neymar
Muhimbili yapongezwa kwa kutoa huduma bora