Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepongezwa na Serikali kwa juhudi inazofanya za kuboresha huduma, sanjari na kuwawezesha watalaam kusoma ili wapate ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.

Pongezi hizo za Serikali zimetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.

Dkt. Mpoki amesema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na uongozi wa hospitali na kwamba hatua hiyo inaleta faraja kwa Watanzania kwani sasa wana uhakika wa kupata huduma bora .

“Naona mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji, Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha  huduma zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu  mna watalaam wengi waliobobea hapa,’’ amesema Dkt. Mpoki.

Kuhusu kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate ujuzi .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.

Dkt. Mpoki ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dk. Doroth Gwajima pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo vyumba vya upasuaji, wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya watoto.


Video: Lover Boy haukuwa wimbo wa Barnabas, D – Classic afunguka yaliyonyuma ya pazia kuhusu wimbo huo

Man City kumkosa Aguero kwa wiki nne
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 30, 2017