Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wanaangalia uwezekano wa kuipata huduma ya winga wa Barcelona, Raphinha ili  akawe mbadala wa winga wao Riyad Mahrez, atakayejiunga na Al-Hilal katika siku chache zijazo.

Man City imekubali kumuuza Mahrez mwenye umri wa miaka 32 kwa Pauni 30 milioni baada ya staa huyo kuomba sana kuondoka kutokana na mshahara mkubwa aliowekewa mezani na Waarabu hao.

Awali, Al Hilal iliwasilisha ofa Pauni 18 milioni ikakataliwa na baada ya majadiliano ya haraka ikatuma ofa ya pili ya Pauni 30 milioni.

Raphinha ambaye alijiunga na Barca mwaka jana akitokea Leeds United kwa ada ya uhamisho ya Euro 58 milioni, alikuwa akihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita la majira baridi ikiwa ni katika mpango wa Barca kutaka kukusanya pesa itakazozitumia kwenye usajili wao.

Msimu uliopita Raphinha mwenye umri wa miaka 26 alicheza mechi 50 za michuano yote, akafunga mabao 10 na kutoa asisti 12.

Ihefu FC wameanza mdogo mdogo Mbeya
Alhaj Dkt. Mwinyi ahimiza uzingatiaji suala la elimu