Mbali na Raheem Sterling kupachika mabao mawili yalioipa uongozi Manchester City kwa muda wa dakika 81 hayakutosha kuwapa alama tatu muhimu mbele ya Wolves kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Sterling alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 25 ambayo ilipanguliwa mwanzo na mlinda mlango wa Wolves kabla ya Sterling kukutana nao mara ya pili na lile la pili alipachika dakika ya 50.
Iliwabidi Wolves kusubiri mpaka dakika ya 55 kupata bao la kwanza kupitia Kwa Adama Traora na dakika ya 82 Raul Jimenez kuweka mzani sawa na dakika ya 89 Matt Doherty alipachika bao la ushindi na kupata jumla na alama tatu muhimu.
Ushindi huo unaofanya Manchester City iliyo chini ya Pep Guardiola kusalia nafasi ya tatu na pointi zake 38 huku Wolves ikiwa nafasi ya tano na alama zake 30 wote wamecheza mechi 19.
City ambao ni mabingwa watetezi wameachwa kwa jumla ya pointi 14 na vinara Liverpool wenye alama 52 na mchezo mmoja mkononi.