Manchester City wanaendelea kuchunguza uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, lakini kipengele chake cha kuachiwa kwa pauni milioni 63 kwa mkupuo mmoja kinaonekana kuwa kikwazo, kwa mujibu wa Sky Sport.
City hawana wasiwasi wowote juu ya bei ya Haaland, lakini kikosi cha Pep Guardiola kingependelea kuepuka kulipa kiasi hicho kwa pamoja.
Man City wanajipanga kufanya makubaliano na Dortmund ambayo yatawawezesha kulipa kidogo zaidi ya hicho, lakini kurefusha malipo kwa muda fulani.
Sehemu ya mbinu ya City inatokana na ada kubwa za wakala ambazo lazima zilipwe kwa Mino Raiola na babake Haaland.
City pia wameweka wazi kuwa hawataki kumlipa Haaland zaidi ya mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa Kevin De Bruyne, ambaye mkataba wake una thamani ya takriban pauni 450,000 mara tu nyongeza zitakapoongezwa.
Kuna matumaini katika Uwanja wa Etihad kwamba City wanaweza kuchukua fursa ya kutokuwa na uhakika kutoka kwa wawindaji wenzao Real.
Los Blancos wanatanguliza saini ya Kylian Mbappe na sasa wanahaha kumtafuta fowadi mwingine mwenye hadhi ya juu huku Karim Benzema mwenye umri wa miaka 34, akiendelea kucheza katika kiwango kinachokaribia kustahili Ballon d’Or.