Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Sadio Mane amejinyakulia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kufunga magoli na kucheza kwa kiwango kizuri katika mechi za mwanzo wa ligi msimu huu.
Mane amefunga katika mechi zote ambazo Liverpool imecheza msimu huu akianza kufunga katika mchezo dhidi ya Watford uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3, kisha katika mchezo wa pili akafunga bao pekee dakika ya 73 lililoipa Liverpool ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Katika mchezo ambao Liverpool iliwachapa Arsenal mabao 4-0 Sadio Mane alikuwa mmoja kati ya safu kali ya ushambuliaji iliyopeleka kilio kwa vijana wa Arsene Wenger baada ya kufunga bao huku mabao mengine yakifungwa na Roberto Firmino na Mohamed Salah.
-
Familia yamrejesha Bony Swansea City
-
Man City, Man United zapinga usajili ‘EPL’ kufungwa mapema
-
Dirisha la usajili Uturuki kumuokoa Jack Wilshere
Mshambuliaji huyo raia wa Senegal ameshinda tuzo hiyo awapiku Phil Jones, Romelu Lukaku, Henrikh Mkhitaryan wote kutoka Manchester United, Alvaro Morata kutoka Chelsea, Jonas Lossl kutoka Huddersfield pamoja na mchezaji mwenzake wa Liverpoo Mohamedl Salah.
Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi tangu aingie katiak ligi kuu ya Uingereza mwezi Septemba mwaka 2014 akitokea klabu ya Red Bull Salzburg ya nchini Austria.