Maporomoko ya ardhi yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo yamesabanisha vifo vya mamia ya watu katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.

Baadhi ya barabara za jiji hilo ziligeuka kuwa mito ya tope lililotokana na maporomoko ya ardhi kutoka milimani.

Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Victor Bockarie Foh amesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kuwa mamia wamepoteza maisha kwa kufunikwa na udongo. Ameongeza kuwa maeneo mengi ya makazi yameharibiwa vibaya kwa kusombwa na tope zito.

Watu mbalimbali wamekuwa wakiweka picha na vipande vya video mitandaoni kuonesha tukio hilo baya.

Vyombo vya habari nchini Sierra Leone vimeripoti kuwa zaidi ya miili 200 iliyotolewa kwenye tope imepelekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti katika hospitali mbalimbali.

Wananchi wakibeba mizigo yao baada ya maporomoko

Sierra Leone imekuwa ikikubwa na tatizo la mafuriko ambapo nyumba zisizokuwa imara zimekuwa zikisombwa na mafuriko hayo na kuwaacha wananchi wakiwa hawana sehemu za kuishi.

Mwaka 2015, mafuriko yalisababisha vifo vya watu 10 na kuwaacha maefu wakiwa hawana makazi.

Majaliwa: Acheni kuajiri watoto kwenye mashamba ya Tumbaku, akemea mimba za utotoni
Ronaldo Hatarini Kufungiwa