Hali mbaya ya mmonyonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo udhalilishaji unaoendela katika katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, imetajwa kuwa ni matokeo ya watu kushindwa kulea na kutibu maradhi ya nafsi na kuelekeza mambo mema yanayotokana na muongozo wa Dini.

Hayo yamebainishwa hii leo Januari 6, 2023 na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman mara baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa wakati akiwasalimia waumini wa Dini hiyo huko Msikiti Nambari Vikokotoni Wilaya ya mjini Unguja.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akisalimiana na Viongozi na waumini wa Dini ya Kiislam.

Amesema, njia pekee ya kuikabili hali hiyo ni kuwepo jitihada kubwa za pamoja kwa jamii katika kuwalea vyema na kuwafunza watoto katika kuendeleza maadili mema na kuwa na ucha MUNGU wa kweli kama muongozo wa dini ya Kiislamu unavyohimiza.

Othman ameongeza kuwa, maelezi mema kwa watoto ndio yanayotoa Vijana na wafuasi wema wenye maadili, watakaoweza kuwa viongozi bora, wakweli na kuchunga haki katika utekelezaji wa majukumu na dhamana mbalimbali.

Rais Biden awashangaa Wabunge, asema ni aibu
Majasusi UN waanika siri za waasi M23