Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP. Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na kumuhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP. Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi, Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Kamanda Muslim.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP. Camillus Wambura.

Aidha, mabadiliko mengine ni pamoja na kumuhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe kuziba pengo la Kamanda Mukama aliyehamishiwa Mkoani Morogoro.

IGP Wambura pia amemuhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi, Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu namba moja Mkoa wa Simiyu, kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa kuchukua nafasi ya Kamanda Mallya aliyehamishiwa Mkoa wa Songwe.

MAAJABU: Talaka yaangamiza familia
Msifiche Mbolea sambazeni kwa Mawakala: RC Mrindoko