Mwanamume mmoja, Michael Haight (42), katika eneo la Utah-Enoch uliopo kati ya Salt Lake City na Las Vegas, amewapiga risasi na kuwaua watoto wake watano, mama mkwe wake na mkewe, kisha ukujiua ikiwa zimepita wiki mbili baada ya mkewe kuwasilisha ombi la talaka.

Michael Haight na mkewe Tausha Haight wakiwa na familia enzi za uhai wao. Picha ya East Idaho News.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi kituo cha Enoch, Jackson Ames amesema Haight alifanya tukio hilo na kwamba kila mhasiriwa alikuwa na majeraha ya risasi huku rekodi za mahakama zikionyesha kuwa mkewe Tausha Haight (40), aliwasilisha kesi ya talaka Desemba 21 na kupewa hati Desemba 27.

Kabla ya tukio hilo, Tausha Haight na familia yake walionekana usiku wa kuamkia siku ya mauaji wakiwa kanisa la wanawake vijana, huku Meya wa mji huo, Geoffrey Chesnut akisema polisi walitumwa nyumbani kwa familia hiyo Jumatano alasiri kwa ukaguzi baada ya mtu kuripoti kuwa Tausha Height alikuwa haonekani kazini.

Waombolezaji wakiweka mdoli na maua nyumbani kwa familia hiyo iliyoaga Dunia kuonesha hisia zao juu ya tukio hilo. Picha ya Mikey Live.

Miongoni mwa waliofariki, ni Watoto wenye umri kati ya miaka 4 hadi 17 wasichana watatu na wavulana wawili, na mwathiriwa mwingine alikuwa mama wa Tausha Haight Gail Earl (78), ambapo katika kesi ya talaka mwakilishi wa Tausha, James Park, alisema hakukuwa na viashiria kuwa mumewe angeweza kutenda tukio hilo.

Washangaa uporaji wa haki za Wanawake
IGP afanya mabadiliko Makamanda wa Polisi