Klabu ya Arsenal imeanza kumfuatilia kwa karibu beki wa kati kutoka England na Crystal Palace, Marc Guehi, wakitaka kumsajili kwa ajili ya kukipiga kwenye kikosi chao msimu ujao.
Arsenal inahitaji huduma ya beki huyo wa kati baada ya sasa kuwa na mashaka makubwa kutokana na hali ya kiafya ya beki wao wa kati, William Saliba.
Beki huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 21, amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo, ambayo aliumia kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Sporting CP miezi miwili iliyopita. Bado haijulikani atarejea ligi uwanjani.
Rob Holding amejaribu kuziba pengo la Saliba wakati huu ambao hayupo, lakini mkataba wa mchezaji huyo utafika tamati mwakani.
Kutokana na hilo, ripoti zinafichua Arsenal sasa imeanza kumtolea macho mchezaji wa zamani wa Chelsea, Guehi ili kuja kuweka mamb sawa huko Emirates.
Guehi amecheza mechi 78 kwenye kikosi cha Palace na Guchi, 22, amecheza mechi 78 kwenye kikosi cha Palace na timu ya taifa ya England imemtumia mara tatu.
Bado haifahamiki Palace itahitaji kiasi gani kwenye mauzo ya mchezaji huyo, lakini kinachoelezwa ni kwamba miamba hiyo ya Selhurst Park itahitaji zaidi ya Pauni 18 milioni ambazo ililipa kupata saini yake mwaka 2021.
Guehi ameanzishwa kwenye mechi zote 33 ilizocheza Palace kwenye Ligi Kuu England msimu huu na muda wote yupo tayari, wakati Saliba ametibua mambo huko Arsenal baada ya kuwa majeruhi katika kipindi muhimu cha timu hiyo kwenye mbio zao za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England.