Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris St-Germain wamepata nguvu baada ya kupokea taarifa njema za kurejea kwa kiungo kutoka nchini Italia Marco Verratti, kuelekea katika mchezo wao wa ligi ya mbingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora.

Kiungo huyo alicheza kwa dakika 60 za mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Bordeaux waliokubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri, na kisha alilazimika kutolewa nje  kufuatia majeraha ya kiazi cha mguu.

Wakati PSG wakifarijika na kurejea kwa kiungo huyo, hii leo watawakosa viungo Thiago Motta (anaetumikia adhabu) na Javier Pastore (majeruhi).

Kwa upande wa wapinzani wao FC Barcelona, beki wa kati Gerard Pique anatarajiwa kucheza baada ya kukosa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Alaves.

Barca wataendelea kuikosa huduma ya beki wa pembeni Aleix Vidal ambaye alipatwa na majeraha ya kifundo cha mguu mwishoni mwa juma lililopita, na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitano.

Mchezo wa hii leo kati ya FC Barcelona na PSG, utakua unakumbushia mpambano wa wawili hao walipokutana katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2015, na Barca walifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1, pia wababe hao wa Cataluña waliwahi kusonga mbele mwaka 2013 dhidi ya PSG kwa faida ya bao la ugenini.

Mshauri Mkuu wa Trump ajiuzulu rasmi
Mamelodi Sundowns Wamsajili Fares Hachi