Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kulipwa Pauni 350,000 kwa juma ambazo ni sawa na shilingi 1,066,719,500 za Kitanzania.
Rashford anatarajiwa kutangazwa kusaini mkataba huo mpya wakati wowote kuanzia sasa.
Mshambuliaji huyo amekubali kusalia ndani ya kikosi hicho licha ya kutakiwa na Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain.
Mkataba huo imeelezwa utakuwa ni mrefu wa kuendelea kusalia ndani ya kikosi hicho cha Manchester United.
Katika mkataba huo mpya, kwa juma Rashford atakuwa akilipwa kiasi cha Pauni 375,000 (Sh 1,066,719,500 za Kitanzania), kwa mwaka atachukua kiasi cha Pauni 19,500,000 (Sh 59,431,515,000 za Kitanzania).
Staa huyo kwa sasa ndiye atakuwa anaongoza kwa mshahara mnono kikosini hapo, baada ya David de Gea kumaliza mkataba wa awali ambao alikuwa akilipwa kiasi hicho cha fedha kwa juma.