Korea Kaskazini imetishia kuishambulia na kuisambaratisha Marekani endapo itadiriki kuiingilia nchi hiyo katika mpango wake wa utengenezaji wa silaha za nyuklia ambao imekuwa ikiendelea nao.

Mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa Marekani ndiyo iliyosababisha kuwekwa kwa vikwazo na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini hivyo kama itaendelea kuichokoza basi itakumbana dhoruba ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Aidha, mvutano kati ya Korea Kaskazi na Marekani umezidi kuchukua sura mpya kila kukicha kufuatia mpango wa Korea Kaskazini kuendelea na mpango wake wa kutengeneza sila za nyuklia.

“Hatua zitazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo haijawai kushuhudiwa katika historia yake, ni bora ikaendelea na shughuli zake na si kuichokonoa Korea Kaskazini,” amesema Han Tae Songhuo huko Geneva

 Hata hivyo, balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa amevikataa vikwazo vyote vilivyowekwa na Baraza hilo huku akisema kuwa vimewekwa kinyume cha sheria.

 

Edinson Cavani avunja rekodi ya Ibrahimovic
Jaffar Iddy: Aliotubeza wameumbuka