Katibu Mkuu wa Shirika la kujihami la nchi za magharibi Nato, Jens Stoltenberg amesema kuwa mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ni tisho kwa usalama wa dunia nzima, na kama zisipochukuliwa hatua stahiki basi kuna uwezekano wa kuleta madhara makubwa.

Amesema kuwa katika sheria ambazo shirika limejiwekea ni pamoja na ile inayosema kuwa mwanachama mmoja akishambuliwa basi itakuwa limeshambuliwa shirika zima hivyo, kutanabaisha kwa kile kinachoendelea Korea Kaskazini.

Aidha, alipoulizwa kama shirika hilo lina mpango wa kuishambulia Korea Kaskazini amesema kuwa hana uhakika kama watatumia sheria hiyo inayosema kuwa mwanachama mmoja akishambuliwa basi shirika zima limeshambuliwa.

Hata hivyo, ametoa wito kwa Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia huku akisema kufanya hivyo ni ukiukwaji mkubwa wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na ni tishio kwa amani ya dunia.

Maswali 10 yanayomkabili dereva wa Lissu
LIVE IKULU: Rais Magufuli amwapisha Jaji MKuu, Profesa Ibrahim