Marekani imeahidi kusaidia katika upelelezi juu ya kutoweka kwa mwandishi wa habari nchini Saudi Arabia katika mazingira ya kutatanisha.
Jamal Khashoggi ni mwandishi wa habari ambaye amekuwa ni mkosoaji mkubwa wa mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman na alionekana kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita, akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia Arabia, jijini Istanbul nchini Uturuki.
Aidha, Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema kuwa Marekani ipo tayari kuwatuma maafisa wa Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (FBI) kusaidia katika upelelezi wa aina yoyote unao hitajika.
Hata hivyo, Maafisa wa Uturuki ambao wameanzisha upelelezi wa kina kuhusu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari, wanasema kwamba wana Imani aliuwawa ndani ya ubalozi, madai ambayo Saudi Arabia inasema hayana msingi wowote.
-
Marekani kusaidia kumtafuta mwandishi wa habari aliyepotea
-
Kim-Joung-un amwalika Papa
-
Kimbunga Michael kuikumba Marekani