Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza usitishwaji wa mchango wa fedha wa Marekani kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) ndani ya siku 30 zijazo ikiwa shirika hilo halitafanya maboresho yanayotakiwa.
Rais Trump ambaye ameendelea kukosoa Shirika hilo ametoa mwezi mmoja kwa WHO kupata matokeo muhimu la sivyo atasitisha kwa muda mchango wa fedha na uanachama wa Marekani kwa Shirika hilo.
Hata hivyo Marekani imelishutumu Shirika hilo kwa kushindwa kuudhibiti na kupuuzia hatari ya ugonjwa wa Corona ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.
Waandishi wa Kenya wakamatwa Arusha
Mwaka 2018-19 Marekani ilichangia takriban Dola milioni 900 kwenye bajeti ya Shirika la Afya. Mchango huo ni sawa na 1/5 ya bajeti nzima ya Shirika hilo kwa kipindi hicho ambayo ni Dola Bilioni 4.4.
Mlipuko wa Corona tayari umeua zaidi ya watu 316,000 ulimwenguni, na Marekani ndiyo nchi iliyoathiriwa zaidi ikiwa na vifo takribani 90,000.